Friday, 10 June 2016

Unknown

EXCLUSIVE: BAADA YA RICH MAVOKO SASA WCB YAMUMEZEA MATE MSANII TAJIKA KUTOKA MOMBASA. JE, NI NANI




Ni juzi tu ambapo kundi zima la WCB wakiongozwa na Diamond Platnumz walitangaza kumsajili Rich Mavoko ambapo msanii huyo alikua msanii wa tatu kujiunga na lebo hio ya Wasafi baada ya Harmonize kufwata na Raymond ambaye alikua "Dancer" wa Diamond.
Kikundi hicho kimeonesha umahiri kwani kila kukicha sifa kede kede zinazidi kukiweka kikundi hicho ambacho kwa sasa ndio kikundi bora East Africa na Afrika kwa jumla kwani sifa zake si Afrika pekee bali ulimwengu mzima.
WCB ni kikundi ama "serikali" ambayo kwa uhakika hakuna msanii yeyote Afrika ambaye hangependa kusajiliwa kwa lebo hio. Ni furaha ya kila msanii angalau siku moja "Majina" yake yatambulike mbele ya viongozi wa kikundi hicho.


Hivi je, ni msanii gani MOMBASA ungependa siku moja umuone akinawiri ndani ya kikundi hicho?
Je, leo hii WCB iseme inatua Mombasa, ni msanii gani wangemkujia?
Je, watatua #TEMPOZ, #KAYG, #TEEHITS, #NUMBER ONE REC, #JUNGLE MASTERS ama watatua STUDIO gani?
Wewe kama shabiki wa mziki wa pwani ungependa msanii gani kumuona kwenye leo za WCB?
Acha maoni yako kwa kisanduku kidogo cha maoni hapo chini.
Asante.



Subscribe to get more videos :