Tuesday, 26 April 2016

Unknown

Kifo cha Mwimbaji Papa Wemba Chawa Pigo Kubwa Kwa Diamond Platnumz.


Kifo cha Mwimbaji Papa Wemba Chawa Pigo Kubwa Kwa Diamond Platnumz.
Msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz ameoneshwa kustushwa kwake na taarifa za kifo cha mwanamuziki mwenye asili ya Congo Papa Wemba, huku akielezea jinsi walivyokutana siku chache zilizopita na kufanya naye collabo.
Kwenye ukurasa wake wa Facebook Diamond ameelezea huzuni hiyo, huku akitoa taarifa kuwa kulikuwa na mipango mingi ya wao kufanya kazi, lakini mauti yameshafuta mipango hiyo.
“Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halafu ghafla naskia habari ya msiba…Dah! nimesikitika sana. Hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyez Mungu ndiyo mpangaji…Pumzika salama Kiongozi wetu daima tutakukumbuka” aliandika Diamond Platnumz kwenye ukurasa wake wa facebook
Msanii Papa Wemba amefariki dunia jana baada ya kuanguka akiwa jukwaani akiimba na kufariki papo hapo nchi Ivory Coast.

 HIVI NDO ALISEMA DIAMOND.
" Jus four weeks ago we were in Paris, featured me in his song and we planned alot for the song and Suddenly got the news....dah! still don't want to believe that you are really Gone Legend....We will always miss you 🙏... ‪#‎RipPapaWemba‬
(Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, Akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halaf ghafla naskia habari ya Msiba...Dah! nimesikitika sana, Hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyez Mungu ndio Mpangaji...Pumzika salama Kiongozi wetu daima tutakukumbuka🙏 #RipPapaWemba )".

Subscribe to get more videos :