Wednesday 20 July 2016

Unknown

BASATA KUGONGA HODI TENA KWA MKALI WA MICHANO NEY WA MITEGO NA KUUFUNGIA WIMBO WAKE MPYA "PALE KATI PATAMU" MP3 HIII HAPA DONDOSHA


WIMBO ULIOFUNGIWA HUU HAPA PALE KATI PATAMU.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na Msanii Ney wa Mitengo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.
Taarifa iliyotolewa leo na Baraza hilo na kusainiwa na Katibu wake Mtendaji Godfrey Mngereza, imeeleza kuwa msanii huyo amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonesho yenye kukiuka maadili.
Taarifa hiyo imesema kuwa kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.
Katika taarifa hiyo Mngereza amesema “Kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.



Ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo.
Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine.
Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati patamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.
Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni wasio na staha na wanaojipanga kuibomoa jamii.” Imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Mbali na kuufungia wimbo huo, BASATA imesema kuwa itachukua hatua nyingine stahiki za kisheria na kuwataka wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapotengeneza kazi zao

#Courtesy of MSETOEA.COM

Subscribe to get more videos :

3 comments

Write comments
Unknown
AUTHOR
20 July 2016 at 12:16 delete This comment has been removed by the author.
avatar