Wednesday 14 September 2016

Unknown

NEW MUSIC ALERT: NAJUTA By SHEPHERD: Shepherd ni msanii mkali aliekua kwa kikundi cha Shemakinz kilicho vuma kwa ujuzi na utunzi wa nyimbo kali kali kama vile Madam Jessica



Shepherd ni msanii mkali aliekua kwa kikundi cha Shemakinz kilicho vuma kwa ujuzi na utunzi wa nyimbo kali kali kama vile Madam Jessica. Tofauti kidogo zilisambaratisha kikundi hicho na Shepherd akamanage kusimama kama msanii solo.
Kwa jitihadha zake aliweza kutoa Vibao kadhaa kama vile Ukuti Ukuti, Mdogo mdogo ambavyo vilifanya vyema Afrika Mashariki na ya kati.

Msanii huyu ameweza kutambulika kwa ukarimu na bidii zake kwani kila anaye fanya kazi na msanii huyu basi malalamiko kwake pembeni. Ameweza kufanya kazi na wasanii wenzake na pia maproducer kadhaa katika mkoa wa pwani.



Kwa hivi sasa, Shepherd anakuletea wimbo wake mpya kwa jina NAJUTA ambao umetengezwa na producer Tee wa TEE HITS mjini Mombasa. Nilipata kuuskiza wimbo huo ambao kwa kweli mashabiki mkue tayari kwani nina uhakika airwaves atazimiliki na hata chats ataselelea kwa wimbo huo.
Wimbo huo utadondoka uraiani punde Producer wake atapo umalizia mastering kwani kwa sasa Tee Producer ako jikoni kupika HIT nyengine baada ya RINGA yake DAZLAH KIDUCHE.

Kaa mkao wa kula.

Subscribe to get more videos :

1 comments:

Write comments
Anonymous
AUTHOR
9 August 2022 at 04:57 delete

Kindly I need the song 'hebu toka kibandani mwangu' by shemakinz bt no where to be found in all plat forms plz plz indeed this song in all cost

Reply
avatar