Tuesday, 1 November 2016

Unknown

"SIHITAJI MENEJA NAHITAJI USHAURI, NILIFANYA NA MENEJA WATATU LAKINI SIKUONA MATUNDA YAKE", - Mr. Blue asema.


Msanii wa Bongo Fleva Mr. Blue amesema hahitaji kuwa na meneja wa kumsaidia katika kazi zake baada ya kuwa nao mara kadhaa na kutoona mafanikio yake.
Akizungumza katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV, Mr. Blue aliweka bayana kwamba hawezi kuishi katika tasnia ya mziki bila kuwa na meneja lakini kutokana na kuona mchango wao kwake haukuzaa matunda kama alivyotegemea akaamua kujiweka pembeni.



"Mimi nilikua siwezi kuendesha maisha yangu ya muziki bila meneja na nilifanya kazi chini ya meneja watatu, lakini kwa sasa nimesema basi sihitaji meneja tena bali nahitaji ushauri wa wadau namna ya kuboresha kazi zangu," asema Mr. Bayser.
Vile vile alisema hana mpango wa kuachia ngoma mwaka huu na hivyo basi aliwaahidi mashabiki wake kwamba atakua akiachia wimbo mmoja kwa mwaka.
Anacho omba msanii huyu ni sapport kwa kazi yoyote ya msanii. Alionyesha ushirikiano wake na Ali Kiba kwa kusapport wimbo wa Abby Skills unaokwenda kwa jina AVERINA.



Subscribe to get more videos :