Friday, 14 October 2016

Unknown

#RadioKayaTupo FamilyFunDay: INATUA MARIAKANI JUMAMOSI TAREHE 15/10/2016 kuanzia saa nne Asubuhi. Zawadi KemKem zitapeanwa siku hiyo. Kuja upate fursa ya kumuona ana kwa ana presenter unae muenzi.


Radio Kaya ni kituo kimoja cha  habari cha hapa mkoani pwani. Ni station moja ambayo inakua kwa kasi kwani kina kitengo muhimu ambacho kinaleta mashabiki zake sugu pamoja na kusherehekea pamoja na wanahabari wao. Wamekua wakitembelea mkoa baada ya mkoa ambapo mashabiki wanapata fursa pekee ya kujirusha na wanahabari wanao waenzi.
Hivi majuzi walikua kule Malindi Gongoni. Hapo kesho Jumamosi Tarehe 15/10/2016, Radio kaya pamoja na kikundi kizima ikiwemo Dj Teddy Mwanamgambo, Sis Shanniez aka Aunty Virus, PPO, na wengine wengi wanatimba mjini MARIAKANI.



Lengo na maudhui ya safari kama hizi ni KUKUTANA NA MASHABIKI wa Radio Kaya. Hapo kutakua na zawadi kem kem ambapo itakua kama #FamilyFunDay ambapo michezo kadhaa itakua. Mshindi atapata fursa ya kurudi nyumbani na zawadi.



Ambia rafiki aambie rafiki kwamba RADIO KAYA inawaletea zawadi MARIAKANI.
Tamasha hilo litakua hapo STEJI YA KALOLENI MARIAKANI. Kuja upate nafasi pekee ya kupiga SELFIE na presenter unaye muenzi.


Kuja ukutane na BLOGGER wako unaye MPENDA.
I will be on stage nikisababisha.
Keep it #AcenaTeq

Subscribe to get more videos :