Wengi wanamuita CRAZY K, msanii kenya ambaye ukija kwa upande wa sanaa ya coast, ni mmoja ya wale tajika kwa utunzi wake nadhifu na jinsi anavyo yapanga mashairi yake. Alitamba kwa nyimbo kadhaa zikiwemo 'Nimechoka' akimshirikisha Kidis The Jembe, 'Hamnielewi', 'Bla Bla, 'Mic Check', na hivi juzi akatoa SHEREHE aliyofanya Thunder Sound akimshirikisha Susumila Yusuf na Ohzy Tayari Ushajua ngoma ambayo ilifanya vyema sana East Africa.
Swali ni, hivi kunani kati yake na Dazlah Kiduche?
Watu walikua wakishangazwa na posts za hivi majuzi za huyu msanii, wengi wakijiuliza je awe anamlenga Chile Monde ama vipi?
Moja ya zile posts zake ni kama ifwatayo;
"Eti kisa ni mapenzi..dubai show za bure,
Nlitafuna nikatema nkawapa kina Ki***"
New jam coming thro, watanyooka tu!”
Hisia nyingi ziliibuka, watu wakawa na maoni na hata ikapelekea mashabiki wa hawa wasanii wawili kurushiana cheche kali. Wengine wakimshutumu msanii mwenyewe kwa kutowajibika na kutafuta ugomvi. Upande wake Dazlah hakujibu kitu kwani alionekana akiwa busy na mishe zake za kimziki.
Tukio lengine msanii Crazy K akapost tena yafwatayo;
“Eti unavunja steji, dogo bado ongeza ujuzi
Kivipi unajiita star, wwe ni nani hata sikujui, Wakali hawajisifu
dogo
Richie namtambua
Susumila Ohzy ukiwaskia tu utawajua,..
#watanyooka_tu”
Hisia tofauti zikazinduka tena. Wengine wakasema wakati wa kiki umeisha, wengine wakimkosoa Crazy k.
Nakumbuka hapo nyuma, kabla msanii huyu kutoa wimbo wake "HAMNIELEWI" alishawai kosana na mashabiki wa Dazla wa upande wa Likoni, kitendo ambacho kilimfanya yeye hata kukatazwa kupiga show Likoni na pia kuwahi kushukishwa kwenye jukwaa akitumbuiza mashabiki wake huko Likoni kwa sababu ya tofauti zao na Dazlah.
Baada ya hapo akaachilia wimbo huo Hamnielewi, kisha akazama kimziki. Baadhi ya pioneers wa mziki wa mombasa waliingilia kati vurugu hilo na kila kitu ikashuluhiswa.
Hivi sasa Crazy K amerudi tena na punch kali, akidai ni wimbo wake mpya wenye uko jikoni. Kati ya hivi punch ameachilia kama kionjo, je ziko na dhalili ama chembe chembe yoyote ya kumgusa CHILE MONDE? na je, CHILE MONDE ana yapi yakusema??
Tegea hapa hapa kwa mengi zaidi.