Tuesday, 31 May 2016

Unknown

NEW MUSIC ALERT: AMILLION RECORDS YAWAKUTANISHA MKALI WA HIP HOP KAA LA MOTO NA MKALI WA QUEEN OF KINGS SIS P QUEEN.


Muda mfupi tu baada ya mkali Kaa La Moto Kiumbe kutangaza kuchukua likizo fupi ya kimziki, hatua ambayo ilishangaza wengi  na kuacha  mashabiki zake sugu midomo wazi, kitendo ambacho mpaka sasa hakijabainika nini haswa kilifanyika ama kutendeka upande wa mkali huyo.
Kati ya wale walioshangazwa na kuondoka kwa Kaa la moto ni Khalid Produza ambaye ni produza na manager wa mwanadada ambaye anatamba kwa sasa na wimbo wake QUEEN OF KINGS
kwa jina Sis P Queen. Khalid aliitisha kukutana na Kaa La Moto na baada ya mazunguzo yao ya kina "ITS OK" ndo jibu lililo ibuka kwa mazungumzo hayo.

ITS OK ni wimbo mpya uliowashirikisha Kaa La Moto na Sis P Queen ambao umeandaliwa na Produza Khalid ambao unadondoka uraiani hapo tarehe mbili june, 2016 (2/6/2016).

Pata kuskiza kazi hio mpya kwa kila redio station ifikapo tarehe mbili. Request zako zitembee kila station. Lets support good music.

 

Subscribe to get more videos :