Thursday, 30 June 2016

Unknown

TRENDING PHOTO OF THE DAY: HIVI SERIKALI INAFANYA NINI KUENDELEZA KIU ZA TAALUMA KAMA HIZI?


Ni juzi tu wengine walisikika wakipinga vikali mfumo wa 8-4-4 ambao unatumika kwa masomo ya Kenya. Wengine wakilia masomo ya sekondari yapunguzwe kwani yaonekana kuwa mzigo na kulemea wanafunzi.
Wengine wakilinganisha masomo ya nchi za nje hasa za ulaya na hapa nchini Kenya. Kuna wale waliosikika wakisema wanafunzi wafundishwe nyadifa tofauti ambapo mwanafunzi akifanya vyema na kuonesha utendakazi mzuri kwa kitengo flaani basi bila kupoteza muda wake mwingi apelekwe chuoni kunako fundishwa taaluma ile.
Sasa kuna wale ambaao huonesha nyota yao kutoka udogoni kama tunavyoona kwa picha hapo juu, ni dhahiri huyu mtoto angependa sana kufanya somo la "Engineering" ambako atakua akizinoa barabara wakati wa ujenzi wake.
Kwa maoni yangu ningependa kupendekeza mfumo wa elimu ya Kenya ubadilishwe kisha wanafunzi wafundishe nyadhifa zile ambazo ziko kwa mipango yao ya kimaisha.

Wewe kama MKENYA, kwenye swali letu la siku;
JE, UNGEPENDEKEZA LIPI KWA MFUMO HUU WA ELIMU WA 8-4-4?

Subscribe to get more videos :