Thursday 29 September 2016

Unknown

NEWS JUST IN: SPONSOR ACHOMWA KISU BAMBURI. Vijana Tumechoka Na Hawa Masponsor. Wanatuibia Rizik Zetu.


Ukiskia uswahilini kuna vituko basi jua maisha ya huku hayaishi purukushani za kila mara.
Nduru ziliskika zikitoka kwa chumba cha msichana mmoja mtaani Bamburi hapo jana jioni. Umati wa watu ulimiminika kwa eneo la tukio hapo ndo walipata milango ya bedsitter hio imefungwa ndani ni wanaume wawili na msichana mmoja.
Chumba cha wairimu (sio jina lake la kweli) kilitapakaa damu kila mahali huku sakafuni pakiwa na mwili wa mtu wa makamo matumbo nje.
Msichana alipiga nduru za kuitisha msaada lakini majirani walimjua kwa ukatili wake, hivyo basi nungunu zilisheheni nje ya kwamba msichana huyo mwenye umri wa 22 alikua na tabia ya kuchezea wanaume wengi wao wakiwa mabwana za watu.
Kijana mwenye hamaki alionekana akiwa na kisu mkononi ambacho alikitumia kumchoma mzee huyo mara kadhaa kisha kutaka kumuua msichana huyo. Aliskika akisema "ningekuua lakini ni vile nakupenda wairimu."
Kisha alifungua mlango umati ukatapakaa ili kumpisha kwani alikua amejaa damu huku kisu hicho kikiwa mkononi. Alipotoka alielezea kilichotokea kwa haraka kisha akapanda pikipiki iliokua yapita na kutokomea kabisa.



Alichoelezea ni hii hapa: -
"Nilikua kwa nyumba na mpenzi wangu ambaye ni mpenzi wangu wa mda mrefu sana. Kisha baada ya kama masaa mawili hivi, kuna mtu alibisha tena bila karibu akaingia mpaka ndani. Hello sweetie ndo maneno yaliyotokea kwa kinywa chake. Kisha akamfikia ili kumkumbatia lakini wairimu akalenga. Hapo ndo niliona hofu kubwa ikiwa ndani yake. Mikononi Sponsor huyo ambaye nilikuja kujua baadae kuwa yeye ndo alikua akimtia kichwa ngumu Wairimu alikua amebeba mfuko wa zawadi kadhaa huku akiwa amebeba nyama nusu.
Kisha akanigeukia akaniuliza na wewe ndo nani. Nikamwambia mimi ni mpenzi wake msichana huyu. Akamgeukia na kumkaripia Wairimu akidhai kuambiwa mimi ni nani na kwa nini niko hapo.  Nikamuambia Wairimu amwambie mimi ni nani lakini hofu yenye alikua nayo akawa hata kutamka maneno hawezi. Sponsor akadaisha kutolewa kwangu kwani yeye ndo anagharamikia kila kitu. Hapo ndo hasira ikanipanda nikamwambie mumetunyanyasa vya kutosha MASPONSOR nyinyi basi leo nitakufanya kitendo hujawai ona. Kisha sponsor akadhai anaweza kunipoteza nisionekane hata ukucha. Nikainuka nikachukua kifunguo cha mlango nikafunga nikatia ufunguo mfukoni kisha nikaenda kitcheni nikatoka na kisu.
Kuona vile sponsor akanirukia ili kisu kidondoke, hakujua mimi mtoto haramu kazi hizi ni zetu wakongwe. Nikamchoma kisu tumboni nikararua kila kitu nikaliangusha huko chini. Nikamgeukia Wairimu nikamchapa kisha huruma ikaniingia nikamuacha.
Wee me nalenga. Makarao wakifika wambieni wasinitafute mananke hawatanipata."



Hapo alipanda boda na kuondoka. Wairimu alitoka nje kuitisha msaada lakini wapi, majirani walishamshiba. Akapigia marafiki zake ambao walifika na kubeba mzee huyo kumpeleka hospitali.

Je, lini masponsor wataacha kunyanyasha vijana wetu? Hili liwe funzo kwa masponsor wote.


#AsanteReporterWanguPandeZile

Subscribe to get more videos :