Tuesday 26 July 2016

Unknown

PRODUCER LAMECK WA NEPTUNE RECORDS AONGELEA KUHUSU SWALA ZIMA LA "KIKI" HUKU AKIGUSIA SIS P NA DAZLAH


Hii ni picha ambayo ilipelekea mtandao kwa jumla kuwaka moto huku cheche za comments zikitiririka kutoka kwa tasnia nzima ya sanaa ya pwani kwani si mashabiki pekee waliojipata kwa mshangao huo bali hata mapresenters na wamiliki wakubwa wa sanaa hio kupigwa na butwaa kwani jambo hilo liliwafungua vinywa watu wengi.
Uchoyo ndo jina la NYIMBO ambayo picha hii inabenua. Maswali tata yaliibuka huku wengine wakinyosha kidole cha lawama kwa mtayarishaji wa PINI hilo ambalo litadondoshwa mnamo tarekhe 1-8-2016.
Kwa maadili mema kwa jamii hii ilionyesha tayari wengi walishaipiga teke kwani tasnia nzima hawakua wametarajia jambo kama hilo kufanyika haswa pwani ambako sanaa yake haijafikia kiwango hicho kwani producer na wasanii wake tayari walikua wamechukua hatua nane mbele.



Pite pite zetu tuliongea na Producer wa Neptune Records, Producer Lameck na alikua na haya yakusema: -

"
Mimi binafsi sina chuki na msanii ama producer yoyote na wala huwa sifatilii mambo yasiyo na faida, nachokifikiria ni jinsi gani nitakuza vipaji vya wasanii wanaochipuka na hata walio bobea, nikimaanisha nahitaji kufanya kitu ambacho kitafurahisha shabiki na hata presenter pia. Kivyangu sitafuti kiki pekee, natafuta cords, snare, hats, strings, bass, tombs, ili kuunda mziki mzuri.

 

Swala la Sis p na Dazla naweza sema kuna vitu zengine mtu anaweza kosea ikawa inaeleweka , na mtu akakosea kwa makusudi so ikiwa niukweli chenye amefanya then sioni ikiwa ni vizuri, kwa sababu tusifanye vituko tukifikiria ni industry pekee itaangalia , lakini kuna familia zetu pia wanatuangalia so sioni ikiwa nimtazamo mzuri , koz ikiwa ingekuwa isue poa then watu waingekuwa na dukuduku.
Hivyo basi sijambo jema kwani kile kitafwata ni kila msanii kufanya vituko zaidi ya mwengine ambapo industry itachafuka kisha kidole cha lawama kitakua kwetu sisi maproducer. So mwenye ni director wa hio nyimbo ningeomba jambo kama hilo marufuku kuregelewa na kupewa kipao mbele. Ingekuwa kule kwa wenzetu Tanzania, BASATA wangeifungia."



Haya kazi kwenu wanapwani na Tasnia nzima ya Sanaa ya pwani.


Subscribe to get more videos :