Wednesday 3 August 2016

Unknown

EXCLUSIVE: "MIMI NA BASATA TULIMALIZANA, ENDELEENI KUOMBA WIMBO KWA MEDIA," ASEMA NAY. SOMA NAKALA NZIMA HAPA


Majuma tu mawili yamepita tangu Baraza la sanaa Tz kutangaza rasmi kumfungia msanii wa Hip hop Nay wa mitego, habari ambazo zilipokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa mziki wake, wengine wakipongeza wengine wakipinga madai hayo. Ilimchukua msanii huyo mda kutafakiri kifungo hicho ila sasa amekuja peupe na kutamka maneno haya;

Nikinukuu,


‘Mimi na basata tumeshamalizana kuanzia sasa hivi watu waendee tu ku-request wimbo unaendelea kupigwa media zote mimi na basata tumeyamaliza, wimbo una version mbili na video nne tofauti’
Video ya kwanza itaanza kutoka wiki ijayo, version ya pili ya audio ya ‘pale kati’ ndio ina marekebisho ambayo yalifanywa kutokana na maagizo ya BASATA, wimbo huu hautakuwa na utofauti sana na ule wa mwanzo ila maneno machache tu nimebadili kama walivyotaka.'


Je, iwe Nay na BASATA wakaosha mikono kwa chombo kimoja? Kaa mkao huu huu kwa habari zaidi.


SIKU NJEMA.




 


To advertise with us send mail to dzengoelvis@gmail.com. Call or Whatsapp to 0713791295.



Subscribe to get more videos :