Tuesday 29 March 2016

Unknown

EXLUSIVE: PATA KUZIJUA SABABU TANO KUU ZINAZOCHANGIA WASANII WENGI KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA.



1.KUIGA:Baadhi ya wasanii hasa wanamuziki wamekua wakiongozwa na hisia za wasanii wenzao waliowahamasisha wao kuingia kwenye muziki,wasanii wengi nchini wamekua wakiiga mambo mengi kutoka kwa wanamuziki wa nchi za magharibi hasa marekani,badhii ya mambo hayo ni pamoja na mahadhi ya muziki,mavazi na hata mitindo ya maisha,ni wazi kuwa kuiga huku kusikozingatia hasara na faida kumepelekea wasanii wengi kujikuta wakiiga baadhi ya mambo yasiyo na faida katika maisha yao kama matumizi ya madawa ya kulevya.
2.UKOSEFU WA ELIMU:Ukosefu wa elimu,ikiwemo elimu ya sanaa ni miongoni mwa mambo yanayopelekea wasanii wengi kujiingiza katika wimbi la matumizi ya madawa ya kulevya,kwa msanii mwenye malengo na mipango ya kufika mbali kisanaa kamwe hawezi kujihusishwa na mambo yatakayoathiri sanaa yake au kumharibia sifa mbele ya jamii
3.TAMAA YA FEDHA:Wasanii wengi wamekua na tamaa ya kupata mafanikio ya muda mfupi,kila msanii ana ndoto za kujulikana na kupata umaarufu,kumiliki mali kama nyumba,magari na vitu vingine vya thamani,tamaa ya fedha imekua chachu kwa baaadhi ya wasanii wengi kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevyia
4.KUJIINGIZA KATIKA MAKUNDI YASIYO NA TIJA:Katika miaka ya hivi karibuni,tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika tasnia ya sanaa na burudani,kumekuwepo na makundi au timu miongoni mwa wasanii,wadau na hata mashabiki,makundi haya au timu hizi zimekua zikitoa support kwa kazi za wasanii wanaofungana nao,kwa wasanii ambao wamekua wakijiingiza katika makundi au timu hizi na baadae kutokea migogoro baina yao,wamejikuta wakiporomoka kisanii,kiuchumi na mwisho kujikuta wakijiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.
5.MSONGO WA MAWAZO:

Subscribe to get more videos :