Msanii wa mziki wa kizazi kipya kanda ya pwani sudi boy amesema kutengeneza kiki ili kujipatia umaarufu sio mambo yake.
Akipiga gumzo na #KayaFlavaz, Sudi Boy amesema kuwa aina ya mziki anaofanya una kiki za kutosha kwa hiyo sio lazima kuzua au kutengeza matukio kama wasanii wengine wafanywavyo ili kuongelewa mitandaoni.
Sudi boy ambaye kwa sasa anatamba na kibao 'nalo' alichomshirikisha arrow boy, ametumia fursa hiyo kuchomoa wimbo mpya kwa jina Kamelodi kama kasi ya kumalizia mwaka.
Skiza Nyimbo Mpya Kamelod hapa
Kamelod MP3
Source: KayaFlavaz.
Tags: Dada Viva #LeoBurdani