Thursday 28 April 2016

Unknown

NYOTA NDOGO AWAANDIKIA BARUA WASANII WOTE WA KENYA.


BARUA HII IWAENDEE WASANII WOTE WA KENYA.
kitu nimejifunza katika haya maisha ya mziki niliopo kwa miaka kumi na sita sasa ni hiki.unaweza kucheka na mtu but mtu asikuonyeshe meno ukafikiria nirafiki.kuna wakati niliwai kutafutwa hili nipewe show na aliekua ananitafuta alimpata mwanamziki mwengine kumuuliza kama yupo na number yangu na huyu msanii alikataa kumpa number kwakumwambia hana number yangu alimuomba amtafutie number yangu alimjibu nafkiri nyota yupo nje ya nchi.huyu msanii ni mtu ambae naongea nae kila wakati tunacheka hata kwa simu.jamaa kwakua alimtaka nyota alinipata tulifanya kazi.alafu sio mmoja imetokea wasanii kadhaa naongea nao nacheka nao na sijawai wauliza ila kama mtu atakua anajua alichokifanya atajijua namzungumzia yeye.wasanii nilioanza nao mziki wengine wamepotea hawakumbukwi hata majina hivi jamani si nafaa kumshukuru MUNGU? Kinachoniweka mpaka siku ya leo kimziki ni KUA NAESHIMU WAKUBWA NA WADOGO NA MIMI NIMTU WA KAWAIDA TU mimi na wewe shabiki wangu hatuna tafauti tafauti zetu ni kazi...BARUA ILIKUA HII.


Kitambo ilikua ngumu sana kwa mtu wa mbali kutupata wasanii kwakua waliambiwa hatuna number zake mara yupo nje ya nchi lakini sikuizi mambo rahisi sana.mtu akikutaka anaingia fb ama twiter ama inster na anakupata tu.sikuizi mtu akiambiwa tumuite nyota ndogo atakwenda kwa fb ataview kila ninachokiposti na kujua mimi ni mtu wa aina gani.picha zangu ninachokiandika ndicho kitanipa kazi ama kitaninyima kazi.ukiposti picha zaa ajabu jueni tunafatiliwa na mashabiki na somtimes hawa mashabiki ndio utuunganisha na kazi zwngine.nimepata kazi mbili za nje kwaajili ya fb.WASANII TUENI MAKINI NA TUNACHOPOSTI INAONGEA WEWE NI MTU WQ AINA GANI.

Pata kuskiza wimbo wake  Nyota Ndogo ft Frasha hapa.

Subscribe to get more videos :